Job 25

? AI
1
Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:
2
“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.
3
Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
4
Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?
5
Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,
6
sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform