1 וַֽיִּשְׁבְּת֡וּ na–walisimama שְׁלֹ֤שֶׁת watatu הָאֲנָשִׁ֣ים wanaume הָ֭אֵלֶּה hawa מֵעֲנ֣וֹת kutoka–kujibu אֶת־ [at] אִיּ֑וֹב Ayubu כִּ֤י kwa–maana ה֖וּא yeye צַדִּ֣יק mwenye–haki בְּעֵינָֽיו׃ machoni–mwake פ [p]
Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe.
2 וַיִּ֤חַר na–iliwaka אַ֨ף ׀ hasira אֱלִיה֣וּא ya–Elihu בֶן־ mwana–wa בַּרַכְאֵ֣ל Barakeli הַבּוּזִי֮ Mbuzi מִמִּשְׁפַּ֪חַ֫ת kutoka–familia–ya רָ֥ם Ramu בְּ֭אִיּוֹב kwa–Ayubu חָרָ֣ה iliwaka אַפּ֑וֹ hasira–yake עַֽל־ kwa–sababu–ya צַדְּק֥וֹ kujihesabia–haki נַ֝פְשׁ֗וֹ nafsi–yake מֵאֱלֹהִֽים׃ kuliko–Mungu
Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu.
3 וּבִשְׁלֹ֣שֶׁת na–kwa–watatu רֵעָיו֮ marafiki–zake חָרָ֪ה iliwaka אַ֫פּ֥וֹ hasira–yake עַ֤ל kwa–sababu אֲשֶׁ֣ר kwamba לֹא־ hawaku מָצְא֣וּ pata מַעֲנֶ֑ה jibu וַ֝יַּרְשִׁ֗יעוּ na–walimhukumu אֶת־ [at] אִיּֽוֹב׃ Ayubu
Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu.
4 וֶֽאֱלִיה֗וּ na–Elihu חִכָּ֣ה alisubiri אֶת־ [at] אִ֭יּוֹב Ayubu בִּדְבָרִ֑ים kwa–maneno כִּ֤י kwa–maana זְֽקֵנִים־ wazee הֵ֖מָּה wao מִמֶּ֣נּוּ kuliko–yeye לְיָמִֽים׃ kwa–siku
Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye.
5 וַיַּ֤רְא na–aliona אֱלִיה֗וּא Elihu כִּ֘י kwamba אֵ֤ין hakuna מַעֲנֶ֗ה jibu בְּ֭פִי katika–kinywa שְׁלֹ֥שֶׁת cha–watatu הָאֲנָשִׁ֗ים wanaume וַיִּ֥חַר na–iliwaka אַפּֽוֹ׃ hasira–yake פ [p]
Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.
6 וַיַּ֤עַן ׀ na–alijibu אֱלִיה֖וּא Elihu בֶן־ mwana–wa בַּֽרַכְאֵ֥ל Barakeli הַבּוּזִ֗י Mbuzi וַיֹּ֫אמַ֥ר na–akasema צָ֘עִ֤יר mdogo אֲנִ֣י mimi לְ֭יָמִים kwa–siku וְאַתֶּ֣ם na–ninyi יְשִׁישִׁ֑ים wazee עַל־ kwa–hiyo כֵּ֖ן kwa–hiyo זָחַ֥לְתִּי nilijinyenyekeza וָֽאִירָ֓א ׀ na–niliogopa מֵחַוֺּ֖ת kuonyesha דֵּעִ֣י ujuzi–wangu אֶתְכֶֽם׃ kwenu
Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.
7 אָ֭מַרְתִּי nilisema יָמִ֣ים siku יְדַבֵּ֑רוּ ziseme וְרֹ֥ב na–wingi שָׁ֝נִ֗ים wa–miaka יֹדִ֥יעוּ wafundishe חָכְמָֽה׃ hekima
Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’
8 אָ֭כֵן lakini רֽוּחַ־ roho הִ֣יא hiyo בֶאֱנ֑וֹשׁ katika–mwanadamu וְנִשְׁמַ֖ת na–pumzi שַׁדַּ֣י ya–Mwenyezi תְּבִינֵֽם׃ inawapa–ufahamu
Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.
9 לֹֽא־ si רַבִּ֥ים wengi יֶחְכָּ֑מוּ wana–hekima וּ֝זְקֵנִ֗ים na–wazee יָבִ֥ינוּ wanaelewa מִשְׁפָּֽט׃ hukumu
Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.
10 לָכֵ֣ן kwa–hiyo אָ֭מַרְתִּי nilisema שִׁמְעָה־ nisikilizeni לִּ֑י mimi אֲחַוֶּ֖ה nitaonyesha דֵּעִ֣י ujuzi–wangu אַף־ pia אָֽנִי׃ mimi
“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi; mimi nami nitawaambia lile ninalojua.
11 הֵ֤ן tazama הוֹחַ֨לְתִּי nilisubiri לְֽדִבְרֵיכֶ֗ם maneno–yenu אָ֭זִין niliwasikiliza עַד־ hadi תְּב֥וּנֹֽתֵיכֶ֑ם ufahamu–wenu עַֽד־ hadi תַּחְקְר֥וּן mlipochunguza מִלִּֽין׃ maneno
Nilingojea mlipokuwa mnaongea, nilizisikiliza hoja zenu; mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,
12 וְעָֽדֵיכֶ֗ם na–kwenu אֶתְבּ֫וֹנָ֥ן nilizingatia וְהִנֵּ֤ה na–tazama אֵ֣ין hakuna לְאִיּ֣וֹב kwa–Ayubu מוֹכִ֑יחַ mshindaji עוֹנֶ֖ה anayejibu אֲמָרָ֣יו maneno–yake מִכֶּֽם׃ miongoni–mwenu
niliwasikiliza kwa makini. Lakini hakuna hata mmoja wenu aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa; hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kujibu hoja zake.
13 פֶּן־ msije תֹּ֣֭אמְרוּ mkasema מָצָ֣אנוּ tumepata חָכְמָ֑ה hekima אֵ֖ל Mungu יִדְּפֶ֣נּוּ atamsukuma לֹא־ si אִֽישׁ׃ mwanadamu
Msiseme, ‘Tumepata hekima; Mungu na amthibitishe kuwa mwongo, wala si mwanadamu.’
14 וְלֹא־ na–hakuelekeza עָרַ֣ךְ alielekeza אֵלַ֣י kwangu מִלִּ֑ין maneno וּ֝בְאִמְרֵיכֶ֗ם na–kwa–maneno–yenu לֹ֣א si אֲשִׁיבֶֽנּוּ׃ nitamjibu
Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu, nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.
15 חַ֭תּוּ wameshindwa לֹא־ hawaku עָ֣נוּ jibu ע֑וֹד tena הֶעְתִּ֖יקוּ yameondoka מֵהֶ֣ם kutoka–kwao מִלִּֽים׃ maneno
“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema; maneno yamewaishia.
16 וְ֭הוֹחַלְתִּי na–nilisubiri כִּי־ kwa–sababu לֹ֣א hawaku יְדַבֵּ֑רוּ sema כִּ֥י kwa–sababu עָ֝מְד֗וּ walisimama לֹא־ hawaku עָ֥נוּ jibu עֽוֹד׃ tena
Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya, kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?
17 אַעֲנֶ֣ה nitajibu אַף־ pia אֲנִ֣י mimi חֶלְקִ֑י sehemu–yangu אֲחַוֶּ֖ה nitaonyesha דֵעִ֣י ujuzi–wangu אַף־ pia אָֽנִי׃ mimi
Mimi nami nitakuwa na la kusema; mimi nami nitasema lile nilijualo.
18 כִּ֭י kwa–maana מָלֵ֣תִי nimejaa מִלִּ֑ים maneno הֱ֝צִיקַ֗תְנִי inanisukuma ר֣וּחַ roho בִּטְנִֽי׃ ya–tumbo–langu
Kwa kuwa nimejawa na maneno, nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;
19 הִנֵּֽה־ tazama בִטְנִ֗י tumbo–langu כְּיַ֥יִן kama–divai לֹא־ ambayo–haijafunguliwa יִפָּתֵ֑חַ haijafunguliwa כְּאֹב֥וֹת kama–viriba חֲ֝דָשִׁ֗ים vipya יִבָּקֵֽעַ׃ vitapasuka
ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.
20 אֲדַבְּרָ֥ה nitasema וְיִֽרְוַֽח־ na–nipate–nafuu לִ֑י mimi אֶפְתַּ֖ח nitafungua שְׂפָתַ֣י midomo–yangu וְאֶֽעֱנֶֽה׃ na–nijibu
Ni lazima niseme ili niweze kutulia; ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.
21 אַל־ si נָ֭א tafadhali אֶשָּׂ֣א nitainua פְנֵי־ uso–wa אִ֑ישׁ mtu וְאֶל־ na–kwa אָ֝דָ֗ם mwanadamu לֹ֣א si אֲכַנֶּֽה׃ nitasifu
Sitampendelea mtu yeyote, wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;
22 כִּ֤י kwa–maana לֹ֣א si יָדַ֣עְתִּי ninajua אֲכַנֶּ֑ה kusifu כִּ֝מְעַ֗ט kwa–upesi יִשָּׂאֵ֥נִי angenichukua עֹשֵֽׂנִי׃ Muumba–wangu
kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza, Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.