Psa 1

? AI
1
Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2
Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.
3
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.
4
Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5
Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6
Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform