Psa 16

? AI
1
Utenzi wa Daudi. Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia.
2
Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.”
3
Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
4
Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu.
5
Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.
6
Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri.
7
Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.
8
Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
9
Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama,
10
kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11
Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform