Psa 47

? AI
1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2
Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
3
Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu.
4
Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda.
5
Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta.
6
Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7
Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa.
8
Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
9
Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform