Psa 61

? AI
1
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu.
2
Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi.
3
Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui.
4
Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.
5
Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.
6
Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi.
7
Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.
8
Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform