Psa 67

? AI
1
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,
2
ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.
3
Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.
4
Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.
5
Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.
6
Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.
7
Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform