1 לַמְנַצֵּ֬חַ Kwa–mwimbaji-mkuu עַֽל־ kuhusu שׁוֹשַׁנִּ֬ים yungiyungi לְדָוִֽד׃ ya–Daudi הוֹשִׁיעֵ֥נִי Uniokoe אֱלֹהִ֑ים Mungu כִּ֤י kwa-maana בָ֖אוּ yameingia מַ֣יִם maji עַד־ hadi נָֽפֶשׁ׃ nafsi
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni.
2 טָבַ֤עְתִּי ׀ Nimezama בִּיוֵ֣ן katika–matope מְ֭צוּלָה ya-kina-kirefu וְאֵ֣ין na–hakuna מָעֳמָ֑ד mahali-pa-kusimama בָּ֥אתִי nimeingia בְמַעֲמַקֵּי־ vilindini מַ֝֗יִם vya–maji וְשִׁבֹּ֥לֶת na–mafuriko שְׁטָפָֽתְנִי׃ yamenizamisha
Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha.
3 יָגַ֣עְתִּי Nimechoka בְקָרְאִי֮ kutoka–kuita נִחַ֪ר kimekauka גְּר֫וֹנִ֥י koo-langu כָּל֥וּ yameisha עֵינַ֑י macho-yangu מְ֝יַחֵ֗ל nikimngojea לֵאלֹהָֽי׃ Mungu-wangu
Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.
4 רַבּ֤וּ ׀ Wamezidi מִשַּׂעֲר֣וֹת kuliko–nywele רֹאשִׁי֮ za–kichwa-changu שֹׂנְאַ֪י wanionichukiao חִ֫נָּ֥ם bure עָצְמ֣וּ wamekuwa-wengi מַ֭צְמִיתַי wanaoniangamiza אֹיְבַ֣י adui-zangu שֶׁ֑קֶר kwa–uongo אֲשֶׁ֥ר yale לֹא־ ambayo–sikuiba גָ֝זַ֗לְתִּי sikuiba אָ֣ז ndipo אָשִֽׁיב׃ ninalazimishwa-kulipa
Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.
5 אֱֽלֹהִ֗ים Mungu אַתָּ֣ה wewe יָ֭דַעְתָּ unajua לְאִוַּלְתִּ֑י upumbavu-wangu וְ֝אַשְׁמוֹתַ֗י na–dhambi-zangu מִמְּךָ֥ kutoka–kwako לֹא־ hazikufichika נִכְחָֽדוּ׃ hazikufichika
Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.
6 אַל־ Wasiaibishwe יֵ֘בֹ֤שׁוּ wasiaibishwe בִ֨י ׀ kwa-sababu-yangu קֹוֶיךָ֮ wanaokungojea אֲדֹנָ֥י Bwana יְהוִ֗ה Yahwe צְבָ֫א֥וֹת wa–majeshi אַל־ wasifedheheshwe יִכָּ֣לְמוּ wasifedheheshwe בִ֣י kwa-sababu-yangu מְבַקְשֶׁ֑יךָ wanaokutafuta אֱ֝לֹהֵ֗י Mungu יִשְׂרָאֵֽל׃ wa–Israeli
Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
7 כִּֽי־ Kwa-maana עָ֭לֶיךָ kwa-ajili-yako נָשָׂ֣אתִי nimebeba חֶרְפָּ֑ה aibu כִּסְּתָ֖ה imefunika כְלִמָּ֣ה fedheha פָנָֽי׃ uso-wangu
Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu.
8 מ֭וּזָר Mgeni הָיִ֣יתִי nimekuwa לְאֶחָ֑י kwa–ndugu-zangu וְ֝נָכְרִ֗י na–mgeni לִבְנֵ֥י kwa–watoto אִמִּֽי׃ wa–mama-yangu
Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.
9 כִּֽי־ Kwa-maana קִנְאַ֣ת wivu בֵּיתְךָ֣ kwa–nyumba-yako אֲכָלָ֑תְנִי umenila וְחֶרְפּ֥וֹת na–matukano ח֝וֹרְפֶ֗יךָ ya–wanaokutukana נָפְל֥וּ yameanguka עָלָֽי׃ juu-yangu
Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.
10 וָאֶבְכֶּ֣ה Na–nililia בַצּ֣וֹם kwa–kufunga נַפְשִׁ֑י nafsi-yangu וַתְּהִ֖י na–ikawa לַחֲרָפ֣וֹת matukano לִֽי׃ kwangu
Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi.
11 וָאֶתְּנָ֣ה Na–nilifanya לְבוּשִׁ֣י mavazi-yangu שָׂ֑ק nguo-za-magunia וָאֱהִ֖י na–nikawa לָהֶ֣ם kwao לְמָשָֽׁל׃ mithali
Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau.
12 יָשִׂ֣יחוּ Wanazungumza בִ֭י kunihusu יֹ֣שְׁבֵי wakaao שָׁ֑עַר langoni וּ֝נְגִינ֗וֹת na–nyimbo שׁוֹתֵ֥י za–wanywao שֵׁכָֽר׃ pombe
Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi.
13 וַאֲנִ֤י Lakini–mimi תְפִלָּתִֽי־ maombi-yangu לְךָ֨ ׀ kwako יְהוָ֡ה Yahwe עֵ֤ת wakati רָצ֗וֹן wa–neema אֱלֹהִ֥ים Mungu בְּרָב־ kwa–wingi חַסְדֶּ֑ךָ wa–upendo-wako-wa-agano עֲ֝נֵ֗נִי unijibu בֶּאֱמֶ֥ת kwa–uaminifu יִשְׁעֶֽךָ׃ wa–wokovu-wako
Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.
14 הַצִּילֵ֣נִי Uniokoe מִ֭טִּיט kutoka–matope וְאַל־ wala–nisizame אֶטְבָּ֑עָה nisizame אִנָּצְלָ֥ה niokolewe מִ֝שֹּֽׂנְאַ֗י kutoka–wanionichukiao וּמִמַּֽעֲמַקֵּי־ na–kutoka–vilindi מָֽיִם׃ vya–maji
Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji.
15 אַל־ Usinizamishe תִּשְׁטְפֵ֤נִי ׀ usinizamishe שִׁבֹּ֣לֶת mafuriko מַ֭יִם ya–maji וְאַל־ wala–usinimeze תִּבְלָעֵ֣נִי usinimeze מְצוּלָ֑ה kilindi וְאַל־ wala–usiniruhusu תֶּאְטַר־ usiniruhusu עָלַ֖י juu-yangu בְּאֵ֣ר shimo פִּֽיהָ׃ lifunge–kinywa-chake
Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.
16 עֲנֵ֣נִי Unijibu יְ֭הוָה Yahwe כִּי־ kwa-maana ט֣וֹב ni-wema חַסְדֶּ֑ךָ upendo-wako-wa-agano כְּרֹ֥ב kwa–wingi רַ֝חֲמֶ֗יךָ wa–huruma-zako פְּנֵ֣ה unigeukee אֵלָֽי׃ mimi
Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie.
17 וְאַל־ Wala–usifiche תַּסְתֵּ֣ר usifiche פָּ֭נֶיךָ uso-wako מֵֽעַבְדֶּ֑ךָ kutoka–mtumishi-wako כִּֽי־ kwa-maana צַר־ nina–dhiki לִ֝֗י mimi מַהֵ֥ר haraka עֲנֵֽנִי׃ unijibu
Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.
18 קָרְבָ֣ה Ikaribie אֶל־ kwa נַפְשִׁ֣י nafsi-yangu גְאָלָ֑הּ uikomboe לְמַ֖עַן kwa-sababu-ya אֹיְבַ֣י adui-zangu פְּדֵֽנִי׃ unikombolee
Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu.
19 אַתָּ֤ה Wewe יָדַ֗עְתָּ unajua חֶרְפָּתִ֣י aibu-yangu וּ֭בָשְׁתִּי na–fedheha-yangu וּכְלִמָּתִ֑י na–udhalilishaji-wangu נֶ֝גְדְּךָ֗ mbele-yako כָּל־ wote צוֹרְרָֽי׃ adui-zangu
Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua.
20 חֶרְפָּ֤ה ׀ Aibu שָֽׁבְרָ֥ה imevunja לִבִּ֗י moyo-wangu וָֽאָ֫נ֥וּשָׁה na–nimezimia וָאֲקַוֶּ֣ה na–nilitazamia לָנ֣וּד huruma וָאַ֑יִן lakini–hapakuwa וְ֝לַמְנַחֲמִ֗ים na–wafariji וְלֹ֣א lakini–sikupata מָצָֽאתִי׃ sikupata
Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata.
21 וַיִּתְּנ֣וּ Na–walinipa בְּבָרוּתִ֣י katika–chakula-changu רֹ֑אשׁ sumu וְ֝לִצְמָאִ֗י na–kwa-kiu-yangu יַשְׁק֥וּנִי walininywesha חֹֽמֶץ׃ siki
Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu.
22 יְהִֽי־ Iwe שֻׁלְחָנָ֣ם meza-yao לִפְנֵיהֶ֣ם mbele-yao לְפָ֑ח mtego וְלִשְׁלוֹמִ֥ים na–kwa-amani-yao לְמוֹקֵֽשׁ׃ tanzi
Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi.
23 תֶּחְשַׁ֣כְנָה Yatiwe-giza עֵ֭ינֵיהֶם macho-yao מֵרְא֑וֹת ili–yasione וּ֝מָתְנֵ֗יהֶם na–viuno-vyao תָּמִ֥יד daima הַמְעַֽד׃ vitetemeke
Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.
24 שְׁפָךְ־ Mwaga עֲלֵיהֶ֥ם juu-yao זַעְמֶ֑ךָ hasira-yako וַחֲר֥וֹן na–ukali אַ֝פְּךָ֗ wa–ghadhabu-yako יַשִּׂיגֵֽם׃ uwafikie
Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.
25 תְּהִי־ Iwe טִֽירָתָ֥ם kambi-yao נְשַׁמָּ֑ה ukiwa בְּ֝אָהֳלֵיהֶ֗ם katika–mahema-yao אַל־ asiwepo יְהִ֥י asiwepo יֹשֵֽׁב׃ mkaaji
Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.
26 כִּֽי־ Kwa-maana אַתָּ֣ה wewe אֲשֶׁר־ uliyempiga הִכִּ֣יתָ uliyempiga רָדָ֑פוּ wanamsaka וְאֶל־ na–juu-ya מַכְא֖וֹב maumivu חֲלָלֶ֣יךָ ya–uliowajeruhi יְסַפֵּֽרוּ׃ wanasimulia
Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.
27 תְּֽנָה־ Ongeza עָ֭וֺן uovu עַל־ juu-ya עֲוֺנָ֑ם uovu-wao וְאַל־ wala–wasiingie יָ֝בֹ֗אוּ wasiingie בְּצִדְקָתֶֽךָ׃ katika–haki-yako
Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako.
28 יִ֭מָּחֽוּ Wafutwe מִסֵּ֣פֶר kutoka–kitabu חַיִּ֑ים cha–uzima וְעִ֥ם na–pamoja-na צַ֝דִּיקִ֗ים wenye-haki אַל־ wasiandikwe יִכָּתֵֽבוּ׃ wasiandikwe
Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.
29 וַ֭אֲנִי Lakini–mimi עָנִ֣י taabu וְכוֹאֵ֑ב na–maumivu יְשׁוּעָתְךָ֖ wokovu-wako אֱלֹהִ֣ים Mungu תְּשַׂגְּבֵֽנִי׃ uniinue
Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.
30 אֲהַֽלְלָ֣ה Nitasifu שֵׁם־ jina אֱלֹהִ֣ים la–Mungu בְּשִׁ֑יר kwa–wimbo וַאֲגַדְּלֶ֥נּוּ na–nitamtukuza בְתוֹדָֽה׃ kwa–shukrani
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
31 וְתִיטַ֣ב Na–itampendeza לַֽ֭יהוָה Yahwe מִשּׁ֥וֹר kuliko–ng'ombe פָּ֗ר dume מַקְרִ֥ן mwenye-pembe מַפְרִֽיס׃ na–kwato
Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.
32 רָא֣וּ Wameona עֲנָוִ֣ים wanyenyekevu יִשְׂמָ֑חוּ wafurahi דֹּרְשֵׁ֥י mnaomtafuta אֱ֝לֹהִ֗ים Mungu וִיחִ֥י na–iishi לְבַבְכֶֽם׃ mioyo-yenu
Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!
33 כִּֽי־ Kwa-maana שֹׁמֵ֣עַ anawasikia אֶל־ wahitaji אֶבְיוֹנִ֣ים wahitaji יְהוָ֑ה Yahwe וְאֶת־ na–wafungwa-wake אֲ֝סִירָ֗יו wafungwa-wake לֹ֣א hawadharu בָזָֽה׃ hawadharu
Bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa.
34 יְֽ֭הַלְלוּהוּ Wamsifu שָׁמַ֣יִם mbingu וָאָ֑רֶץ na–nchi יַ֝מִּ֗ים bahari וְֽכָל־ na–kila רֹמֵ֥שׂ kitambaacho בָּֽם׃ ndani-yake
Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake,
35 כִּ֤י Kwa-maana אֱלֹהִ֨ים ׀ Mungu י֘וֹשִׁ֤יעַ ataokoa צִיּ֗וֹן Sayuni וְ֭יִבְנֶה na–atajenga עָרֵ֣י miji יְהוּדָ֑ה ya–Yuda וְיָ֥שְׁבוּ na–watakaa שָׁ֝֗ם huko וִירֵשֽׁוּהָ׃ na–kuimiliki
kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,
36 וְזֶ֣רַע Na–uzao עֲ֭בָדָיו wa–watumishi-wake יִנְחָל֑וּהָ utairithi וְאֹהֲבֵ֥י na–wapendao שְׁ֝מ֗וֹ jina-lake יִשְׁכְּנוּ־ watakaa בָֽהּ׃ ndani-yake
watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.