Psa 82

? AI
1
Zaburi ya Asafu. Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2
“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
3
Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.
4
Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5
“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika.
6
“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7
Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8
Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform