Psa 96

? AI
1
Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.
2
Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
3
Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
4
Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
5
Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.
6
Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
7
Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.
8
Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake.
9
Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake.
10
Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu.
11
Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
12
mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;
13
itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform