1 הַֽלְלוּיָ֨הּ ׀ Haleluya הוֹד֣וּ shukuruni לַיהוָ֣ה kwa–Yahwe כִּי־ kwa–kuwa ט֑וֹב mwema כִּ֖י kwa–kuwa לְעוֹלָ֣ם milele חַסְדּֽוֹ׃ upendo–wake
Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
2 מִ֗י nani יְ֭מַלֵּל ataweza–kusema גְּבוּר֣וֹת matendo–makuu–ya יְהוָ֑ה Yahwe יַ֝שְׁמִ֗יעַ atafanya–kusikiwa כָּל־ yote תְּהִלָּתֽוֹ׃ sifa–yake
Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana au kutangaza kikamilifu sifa zake?
3 אַ֭שְׁרֵי heri שֹׁמְרֵ֣י wanaoshika מִשְׁפָּ֑ט haki עֹשֵׂ֖ה anayetenda צְדָקָ֣ה haki בְכָל־ wakati–wote עֵֽת׃ wakati
Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema.
4 זָכְרֵ֣נִי nikumbuke יְ֭הוָה Yahwe בִּרְצ֣וֹן kwa–upendeleo–wa עַמֶּ֑ךָ watu–wako פָּ֝קְדֵ֗נִי nijilie בִּישׁוּעָתֶֽךָ׃ kwa–wokovu–wako
Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa,
5 לִרְא֤וֹת ׀ kuona בְּט֘וֹבַ֤ת mema–ya בְּחִירֶ֗יךָ wateule–wako לִ֭שְׂמֹחַ kufurahi בְּשִׂמְחַ֣ת kwa–furaha–ya גּוֹיֶ֑ךָ taifa–lako לְ֝הִתְהַלֵּ֗ל kujisifu עִם־ pamoja–na נַחֲלָתֶֽךָ׃ urithi–wako
ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu.
6 חָטָ֥אנוּ tumetenda–dhambi עִם־ pamoja–na אֲבוֹתֵ֗ינוּ baba–zetu הֶעֱוִ֥ינוּ tumekosea הִרְשָֽׁעְנוּ׃ tumetenda–uovu
Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda uovu.
7 אֲב֘וֹתֵ֤ינוּ baba–zetu בְמִצְרַ֨יִם ׀ katika–Misri לֹא־ hawaku הִשְׂכִּ֬ילוּ elewa נִפְלְאוֹתֶ֗יךָ maajabu–yako לֹ֣א hawaku זָ֭כְרוּ kumbuka אֶת־ (kiapo) רֹ֣ב wingi–wa חֲסָדֶ֑יךָ huruma–zako וַיַּמְר֖וּ na–waliasi עַל־ kwenye יָ֣ם bahari בְּיַם־ kwenye–bahari סֽוּף׃ ya–Shamu
Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.
8 וַֽ֭יּוֹשִׁיעֵם na–akawaokoa לְמַ֣עַן kwa–ajili–ya שְׁמ֑וֹ jina–lake לְ֝הוֹדִ֗יעַ kujulisha אֶת־ (kiapo) גְּבוּרָתֽוֹ׃ nguvu–zake
Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.
9 וַיִּגְעַ֣ר na–akaikemea בְּיַם־ bahari–ya ס֭וּף Shamu וַֽיֶּחֱרָ֑ב na–ikakauka וַיּוֹלִיכֵ֥ם na–akawaongoza בַּ֝תְּהֹמ֗וֹת katika–vilindi כַּמִּדְבָּֽר׃ kama–jangwa
Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.
10 וַֽ֭יּוֹשִׁיעֵם na–akawaokoa מִיַּ֣ד kutoka–mkono–wa שׂוֹנֵ֑א anayechukia וַ֝יִּגְאָלֵ֗ם na–akawakomboa מִיַּ֥ד kutoka–mkono–wa אוֹיֵֽב׃ adui
Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.
11 וַיְכַסּוּ־ na–yakawafunika מַ֥יִם maji צָרֵיהֶ֑ם adui–zao אֶחָ֥ד hata–mmoja מֵ֝הֶ֗ם wao לֹ֣א hakusalia נוֹתָֽר׃ alibaki
Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja.
12 וַיַּאֲמִ֥ינוּ na–wakaamini בִדְבָרָ֑יו maneno–yake יָ֝שִׁ֗ירוּ wakaimba תְּהִלָּתֽוֹ׃ sifa–yake
Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake.
13 מִֽ֭הֲרוּ walifanya–haraka שָׁכְח֣וּ wakasahau מַעֲשָׂ֑יו matendo–yake לֹֽא־ hawaku חִ֝כּ֗וּ ngoja לַעֲצָתֽוֹ׃ shauri–lake
Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake.
14 וַיִּתְאַוּ֣וּ na–wakatamani תַ֭אֲוָה tamaa בַּמִּדְבָּ֑ר jangwani וַיְנַסּוּ־ na–wakamjaribu אֵ֝֗ל Mungu בִּֽישִׁימֽוֹן׃ nyikani
Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani.
15 וַיִּתֵּ֣ן na–akawapa לָ֭הֶם wao שֶׁאֱלָתָ֑ם maombi–yao וַיְשַׁלַּ֖ח na–akatuma רָז֣וֹן udhaifu בְּנַפְשָֽׁם׃ katika–nafsi–zao
Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.
16 וַיְקַנְא֣וּ na–wakaonea–wivu לְ֭מֹשֶׁה Musa בַּֽמַּחֲנֶ֑ה kambini לְ֝אַהֲרֹ֗ן Haruni קְד֣וֹשׁ mtakatifu יְהוָֽה׃ wa–Yahwe
Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.
17 תִּפְתַּח־ ilifunguka אֶ֭רֶץ ardhi וַתִּבְלַ֣ע na–ikammeza דָּתָ֑ן Dathani וַ֝תְּכַ֗ס na–ikawafunika עַל־ juu–ya עֲדַ֥ת kundi–la אֲבִירָֽם׃ Abiramu
Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake.
18 וַתִּבְעַר־ na–ukawaka אֵ֥שׁ moto בַּעֲדָתָ֑ם katika–kundi–lao לֶ֝הָבָ֗ה mwali תְּלַהֵ֥ט ukawachoma רְשָׁעִֽים׃ waovu
Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu.
19 יַעֲשׂוּ־ walifanya עֵ֥גֶל ndama בְּחֹרֵ֑ב Horebu וַ֝יִּשְׁתַּחֲו֗וּ na–wakasujudu לְמַסֵּכָֽה׃ kwa–sanamu
Huko Horebu walitengeneza ndama, na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.
20 וַיָּמִ֥ירוּ na–wakabadilisha אֶת־ (kiapo) כְּבוֹדָ֑ם utukufu–wao בְּתַבְנִ֥ית kwa–mfano–wa שׁ֝֗וֹר ng'ombe אֹכֵ֥ל anayekula עֵֽשֶׂב׃ nyasi
Waliubadilisha Utukufu wao kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.
21 שָׁ֭כְחוּ wakamsahau אֵ֣ל Mungu מוֹשִׁיעָ֑ם mwokozi–wao עֹשֶׂ֖ה aliyefanya גְדֹל֣וֹת mambo–makubwa בְּמִצְרָֽיִם׃ katika–Misri
Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,
22 נִ֭פְלָאוֹת maajabu בְּאֶ֣רֶץ katika–nchi–ya חָ֑ם Hamu נ֝וֹרָא֗וֹת mambo–ya–kutisha עַל־ kwenye יַם־ bahari–ya סֽוּף׃ Shamu
miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.
23 וַיֹּ֗אמֶר na–akasema לְֽהַשְׁמִ֫ידָ֥ם kuwaangamiza לוּלֵ֡י kama–si מֹ֘שֶׁ֤ה Musa בְחִיר֗וֹ mteule–wake עָמַ֣ד alisimama בַּפֶּ֣רֶץ penye–ufa לְפָנָ֑יו mbele–yake לְהָשִׁ֥יב kurudisha חֲ֝מָת֗וֹ ghadhabu–yake מֵֽהַשְׁחִֽית׃ kutoka–kuangamiza
Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.
24 וַֽ֭יִּמְאֲסוּ na–wakakataa בְּאֶ֣רֶץ nchi חֶמְדָּ֑ה ya–kupendeza לֹֽא־ hawaku הֶ֝אֱמִ֗ינוּ amini לִדְבָרֽוֹ׃ neno–lake
Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake.
25 וַיֵּרָגְנ֥וּ na–wakanung'unika בְאָהֳלֵיהֶ֑ם katika–mahema–yao לֹ֥א hawaku שָׁ֝מְע֗וּ sikia בְּק֣וֹל sauti–ya יְהוָֽה׃ Yahwe
Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana.
26 וַיִּשָּׂ֣א na–akainua יָד֣וֹ mkono–wake לָהֶ֑ם dhidi–yao לְהַפִּ֥יל kuwaangusha א֝וֹתָ֗ם wao בַּמִּדְבָּֽר׃ jangwani
Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani,
27 וּלְהַפִּ֣יל na–kuwaangusha זַ֭רְעָם uzao–wao בַּגּוֹיִ֑ם miongoni–mwa–mataifa וּ֝לְזָרוֹתָ֗ם na–kuwatawanya בָּאֲרָצֽוֹת׃ katika–nchi
kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote.
28 וַ֭יִּצָּ֣מְדוּ na–wakajifunga לְבַ֣עַל פְּע֑וֹר kwa–Baal–Peori וַ֝יֹּאכְל֗וּ na–wakala זִבְחֵ֥י dhabihu–za מֵתִֽים׃ wafu
Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.
29 וַ֭יַּכְעִיסוּ na–wakamkasirisha בְּמַֽעַלְלֵיהֶ֑ם kwa–matendo–yao וַתִּפְרָץ־ na–ikaenea בָּ֝֗ם miongoni–mwao מַגֵּפָֽה׃ tauni
Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao.
30 וַיַּעֲמֹ֣ד na–akasimama פִּֽ֭ינְחָס Finehasi וַיְפַלֵּ֑ל na–akahukumu וַ֝תֵּעָצַ֗ר na–ikasimama הַמַּגֵּפָֽה׃ tauni
Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa.
31 וַתֵּחָ֣שֶׁב na–ikahesabiwa ל֭וֹ kwake לִצְדָקָ֑ה kama–haki לְדֹ֥ר kwa–kizazi וָ֝דֹ֗ר na–kizazi עַד־ hadi עוֹלָֽם׃ milele
Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.
32 וַ֭יַּקְצִיפוּ na–wakamkasirisha עַל־ kwenye מֵ֥י maji–ya מְרִיבָ֑ה Meriba וַיֵּ֥רַע na–ikawa–vibaya לְ֝מֹשֶׁ֗ה kwa–Musa בַּעֲבוּרָֽם׃ kwa–sababu–yao
Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao;
33 כִּֽי־ kwa–kuwa הִמְר֥וּ waliudhi אֶת־ (kiapo) רוּח֑וֹ roho–yake וַ֝יְבַטֵּ֗א na–akasema–bila–kufikiri בִּשְׂפָתָֽיו׃ kwa–midomo–yake
kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.
34 לֹֽא־ hawaku הִ֭שְׁמִידוּ waangamiza אֶת־ (kiapo) הָֽעַמִּ֑ים mataifa אֲשֶׁ֤ר ambayo אָמַ֖ר aliamuru יְהוָ֣ה Yahwe לָהֶֽם׃ wao
Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza,
35 וַיִּתְעָרְב֥וּ na–wakachanganyika בַגּוֹיִ֑ם na–mataifa וַֽ֝יִּלְמְד֗וּ na–wakajifunza מַֽעֲשֵׂיהֶֽם׃ matendo–yao
bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao.
36 וַיַּעַבְד֥וּ na–wakaabudu אֶת־ (kiapo) עֲצַבֵּיהֶ֑ם sanamu–zao וַיִּהְי֖וּ na–ikawa לָהֶ֣ם kwao לְמוֹקֵֽשׁ׃ mtego
Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao.
37 וַיִּזְבְּח֣וּ na–wakadhabihu אֶת־ (kiapo) בְּ֭נֵיהֶם wana–wao וְאֶת־ na בְּנֽוֹתֵיהֶ֗ם binti–zao לַשֵּֽׁדִים׃ kwa–mashetani
Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani.
38 וַיִּֽשְׁפְּכ֨וּ na–wakamwaga דָ֪ם damu נָקִ֡י isiyo–na–hatia דַּם־ damu–ya בְּנֵ֘יהֶ֤ם wana–wao וּֽבְנוֹתֵיהֶ֗ם na–binti–zao אֲשֶׁ֣ר ambao זִ֭בְּחוּ walidhabihu לַעֲצַבֵּ֣י kwa–sanamu–za כְנָ֑עַן Kanaani וַתֶּחֱנַ֥ף na–ikauchafua הָ֝אָ֗רֶץ nchi בַּדָּמִֽים׃ kwa–damu
Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
39 וַיִּטְמְא֥וּ na–wakajinajisi בְמַעֲשֵׂיהֶ֑ם kwa–matendo–yao וַ֝יִּזְנוּ֗ na–wakazini בְּמַֽעַלְלֵיהֶֽם׃ kwa–njia–zao
Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.
40 וַיִּֽחַר־ na–ikawaka אַ֣ף hasira–ya יְהוָ֣ה Yahwe בְּעַמּ֑וֹ dhidi–ya–watu–wake וַ֝יְתָעֵ֗ב na–akachukia אֶת־ (kiapo) נַחֲלָתֽוֹ׃ urithi–wake
Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake.
41 וַיִּתְּנֵ֥ם na–akawatia בְּיַד־ mikononi–mwa גּוֹיִ֑ם mataifa וַֽיִּמְשְׁל֥וּ na–wakawatawala בָ֝הֶ֗ם wao שֹׂנְאֵיהֶֽם׃ wanaowachukia
Akawakabidhi kwa mataifa na adui zao wakawatawala.
42 וַיִּלְחָצ֥וּם na–wakawaonea אוֹיְבֵיהֶ֑ם adui–zao וַ֝יִּכָּנְע֗וּ na–wakanyenyekeshwa תַּ֣חַת chini–ya יָדָֽם׃ mkono–wao
Adui zao wakawaonea na kuwatia chini ya mamlaka yao.
43 פְּעָמִ֥ים mara רַבּ֗וֹת nyingi יַצִּ֫ילֵ֥ם aliwaokoa וְ֭הֵמָּה lakini–wao יַמְר֣וּ waliasi בַעֲצָתָ֑ם kwa–shauri–lao וַ֝יָּמֹ֗כּוּ na–wakaanguka בַּעֲוֺנָֽם׃ katika–uovu–wao
Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao.
44 וַ֭יַּרְא na–akaona בַּצַּ֣ר katika–dhiki לָהֶ֑ם yao בְּ֝שָׁמְע֗וֹ wakati–aliposikia אֶת־ (kiapo) רִנָּתָֽם׃ kilio–chao
Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;
45 וַיִּזְכֹּ֣ר na–akakumbuka לָהֶ֣ם kwa–ajili–yao בְּרִית֑וֹ agano–lake וַ֝יִּנָּחֵ֗ם na–akajuta כְּרֹ֣ב kwa–sababu–ya–wingi–wa [חסדו] (Ketiv) (חֲסָדָֽיו׃) huruma–zake
kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.
46 וַיִּתֵּ֣ן na–akawapa אוֹתָ֣ם wao לְרַחֲמִ֑ים huruma לִ֝פְנֵ֗י mbele–ya כָּל־ wote שׁוֹבֵיהֶֽם׃ waliowateka
Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka.
47 הוֹשִׁיעֵ֨נוּ ׀ tuokoe יְה֘וָ֤ה Yahwe אֱלֹהֵ֗ינוּ Mungu–wetu וְקַבְּצֵנוּ֮ na–ukusanye מִֽן־ kutoka–kwa הַגּ֫וֹיִ֥ם mataifa לְ֭הֹדוֹת kushukuru לְשֵׁ֣ם jina קָדְשֶׁ֑ךָ lako–takatifu לְ֝הִשְׁתַּבֵּ֗חַ kujivunia בִּתְהִלָּתֶֽךָ׃ sifa–zako
Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.
48 בָּר֤וּךְ־ abarikiwe יְהוָ֨ה Yahwe אֱלֹהֵ֪י Mungu–wa יִשְׂרָאֵ֡ל Israeli מִן־ kutoka הָ֤עוֹלָ֨ם ׀ milele וְעַ֬ד na–hadi הָעוֹלָ֗ם milele וְאָמַ֖ר na–waseme כָּל־ wote הָעָ֥ם watu אָמֵ֗ן Amina הַֽלְלוּ־ msifuni יָֽהּ׃ Yah
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana.