Psa 130

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2
Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
3
Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4
Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.
5
Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.
6
Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
7
Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.
8
Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform