Psa 146

? AI
1
Msifuni Bwana! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,
2
Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo.
3
Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa.
4
Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
5
Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,
6
Muumba wa mbingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo ndani yake: Bwana anayedumu kuwa mwaminifu milele na milele.
7
Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru,
8
Bwana huwafumbua vipofu macho, Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, Bwana huwapenda wenye haki.
9
Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.
10
Bwana atamiliki milele, Mungu wako, ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Bwana.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform