Psa 99

? AI
1
Bwana anatawala, mataifa na yatetemeke; anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike.
2
Bwana ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote.
3
Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu!
4
Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa.
5
Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu.
6
Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu.
7
Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa.
8
Ee Bwana, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
9
Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform