Psa 100

? AI
1
Zaburi ya shukrani. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
2
Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.
4
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5
Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform