Psa 110

? AI
1
Zaburi ya Daudi. Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2
Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako.
3
Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako.
4
Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”
5
Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6
Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7
Atakunywa maji katika kijito kando ya njia, kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform