Psa 120

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu.
2
Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.
3
Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4
Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5
Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6
Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7
Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform