Psa 121

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi?
2
Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.
3
Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,
4
hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.
5
Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
6
jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7
Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako,
8
Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform