Psa 122

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.”
2
Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.
3
Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.
4
Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.
5
Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
6
Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.
7
Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”
8
Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9
Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform