Psa 126

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2
Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.”
3
Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.
4
Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.
5
Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6
Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform