Psa 127

? AI
1
Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.
2
Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.
3
Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake.
4
Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
5
Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform