Psa 113

? AI
1
Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana.
2
Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele.
3
Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
4
Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu.
5
Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
6
ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi?
7
Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
8
huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
9
Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana.
Global Bible Tools - Collaborative Bible translation platform